Mvulana wa miaka 15 akamatwa kuhusiana na uhalifu Nairobi

Kupitia ukurasa wao wa twitter, idara ya upelelezi wa jinai ilisema kwamba mvulana huyo alikamatwa baada ya kuandamwa

Muhtasari
  • Mvulana huyo alisemekana kuruka ukuta na kuingia kwenye mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Nairobi ili kuepuka kukamatwa
Pingu
Image: Radio Jambo

Maafisa wa kituo cha polisi cha Akila wamemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 15 huku wakiendelea kukabiliana na makundi ya wahalifu Jijini Nairobi.

Kupitia ukurasa wao wa twitter, idara ya upelelezi wa jinai ilisema kwamba mvulana huyo alikamatwa baada ya kuandamwa kwa kilomita sita kwenye barabara ya pembezoni ya Southern by-pass Nairobi.

Mvulana huyo alishukiwa kumpora mwanaume mmoja rununu ya aina ya iphone alipokuwa akitembea kando ya barabara hiyo.

Mvulana huyo alisemekana kuruka ukuta na kuingia kwenye mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Nairobi ili kuepuka kukamatwa.

Polisi walifanikiwa kupata kisu karibu na uwanja wa ndege wa Wilson kinachoaminika kutumiwa na wahalifu kuwadunga wapita njia.

Inaaminika kwamba mshukiwa huyo ambaye ni mkaazi wa Lindi katika mtaa wa mabanda ya Kibra amekuwa akiwavamia wapita njia katika barabara hiyo.