logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jengo lingine la ghorofa 5 laporomoka Ruaka, Kiambu

Mtu mmoja tayari ameokolewa na kufikishwa hospitarini.

image
na Davis Ojiambo

Habari17 November 2022 - 05:31

Muhtasari


  • • Jengo hili ambalo limeanguka karibu na eneo ya  Fortune Club liliangukia nyumba zingine za karibu.
Jengo la ghorofa 5 laporomoka Ruaka, Kiambu

Wakaazi wa Ruaka  eneo la Kiambu, waligutushwa na kuporomoka kwa jengo la ghorofa 5 lilokuwa  likijengwa.

Jengo hili ambalo limeanguka karibu na eneo ya  Fortune Club liliangukia nyumba zingine za karibu.

Kulingana na ripoti za awali mtu mmoja aliokolewa kwenye jengo hilo huku waokoaji wakiendelea kufukua vifusi vya jengo hilo.  Kuna hofu kuwa huenda kuna watu waliokwama ndani ya jengo hilo.

Maafisa wa uokoaji kutoka kaunti ya Kiambu, msalaba mwekundu na idara ya polisi tayari wamefika kwenye eneo la  tukio.

 

Huo ni mkasa wa pili kutokea chini ya wiki moja baada ya jengo la ghorofa 7 kuanguka eneo la Seasons,Kasarani  siku ya Jumanne Novemba 14.

Takriban watu 3 walikufa wakati jengo hilo lilipoporomoka. Watu wengine 6 waliokolewa kutoka kwa vifusi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved