Mvulana,14,apatikana amefariki nyumbani kwao Nairobi

Polisi walisema walipigiwa simu na kufahamishwa kuhusu kupatikana kwa mwili huo kitandani.

Muhtasari
  • Bidan Mburu, mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Zawadi jijini Nairobi alipatikana amefariki katika nyumba yao Jumanne asubuhi
  • Mwili ulikuwa na michubuko na majeraha mgongoni, kifuani na kwenye paji la uso
Crime Scene
Image: HISANI

Sintofahamu imeshuhudiwa kuhusu kifo cha mvulana wa miaka 14 katika mtaa wa California, Nairobi.

Bidan Mburu, mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Zawadi jijini Nairobi alipatikana amefariki katika nyumba yao Jumanne asubuhi.

Mwili ulikuwa na michubuko na majeraha mgongoni, kifuani na kwenye paji la uso.

Familia ilisema mvulana huyo alikuwa nje ya shule kwa wiki tatu kutokana na masuala ya kinidhamu.

Polisi walisema walipigiwa simu na kufahamishwa kuhusu kupatikana kwa mwili huo kitandani.

Timu iliyotembelea eneo la tukio ilisema iliarifiwa mvulana huyo alirudi usiku wa manane Jumatatu akiwa na shati lililochanika huku akionekana kupigwa na kulala na kukutwa amefariki asubuhi.

Haijulikani alikuwa na nani na ikiwa walimpiga. Polisi walisema wanachunguza tukio hilo.

Mwili huo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi zaidi na uchunguzi wa maiti.es