(Video) Mwandishi wa habari apigwa makofi na walizi wa Dorcas Rigathi

Sababu ya kupigwa makofi bado haijafichuliwa.

Muhtasari

• Kwenye video hiyo, walinzi hao walimnyanyasa kwa kumpiga Mwangi kabla ya  kutawanywa na afisa mmoja.

Image: Screengrab

Video ya mwandishi wa habari wa Murang'a Mwangi Muiruri akikabidhiwa kichapo na walinzi wa mkewe Naibu Rais Rigathi Gachagua,Dorcas Rigathi imezua gumzo mtandaoni.

Mwangi alipigwa na walinzi hao kwenye hafla ya kugawa chakula cha msaada ambayo Dorcas alikuwa amehudhuria.

Hafla hiyo iliandaliwa huko Gatanga, Murang'a.

Kwenye video hiyo, walinzi hao walimnyanyasa kwa kumpiga Mwangi kabla ya kuwatanywa na afisa mmoja.

Mtu mwingine anayekisiwa kuwa mwanahabari aliskika akisema kuwa Mwangi ni rafiki yake ili waache kumnyanyasa.

Hayo yalitokea baada ya mwanahabari huyo kutaka kurekodi hafla hiyo.

Walinzi waliompiga mwanahabari huyo walidaiwa kutoheshimu beji ya wanahabari ambayo Mwangi alikuwa nayo kumaanisha alikuwa na ruhusa ya kurekodi kilichokuwa kinaendelea.

Bado haijadhibitika iwapo wanahabari hao walipata majeraha.

Hata hivyo sababu ya wanahabari hao kunyanyaswa bado haijajulikana.

Haya yamejiri miezi michache baada ya mwanahabari wa Nation Media Group kunyanyaswa na watu wasiojulikana huko Migori, Kakrao Shopping Centre.