(+PICHA)Radio Africa Group,wizara ya utalii washirikiana kukuza sekta ya utalii

Quarcoo amesema Radio Africa iko tayari kushirikiana na wizara hiyo ili kuongeza idadi ya watalii.

Muhtasari
  • Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Africa Patrick Quarcoo alisema mashirika ya kibiashara pia yana jukumu la kukuza sekta mbalimbali za uchumi
WAZIRI WA UTALII PENINAH MALONZA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA RADIOAFRICA GROUP PATRICK QUARCOO
Image: ENOS TECHE

Radio Africa Group na Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Urithi wameingia katika ushirikiano unaolenga kuifanya Kenya kuwa kivutio kikuu cha utalii.

Makubaliano hayo yalitimizwa wakati Waziri Peninah Malonza alipoongoza wajumbe kutoka wizarani na kutembelea Radio Africa Groupeneo la Lion Place jijini Nairobi siku ya Ijumaa.

Image: ENOS TECHE

Malonza alisikitika kwamba Kenya haikuweza kutumia kikamilifu uwezo wake wa utalii kwa miaka mingi lakini imejaliwa kuwa na wanyamapori, maeneo ya kihistoria na utamaduni tajiri.

“Tulikuwa tukifanya vizuri sana siku za nyuma tulipokuwa tukiingiza fedha nyingi za kigeni lakini mvua ilianza kutushinda wakati fulani. Sasa tuko katika nambari ya nne na nimeambiwa mifugo imetupita,” Malonza alisema.

MTANGAZAJI MASSAWE JAPANNI NA WAZIRI WA UTALII PENINAH MALONZA KWENYE STUDIO ZA RADIOJAMBO MNAMO 13/01/2023
Image: ENOS TECHE

Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Africa Patrick Quarcoo alisema mashirika ya kibiashara pia yana jukumu la kukuza sekta mbalimbali za uchumi.

“Tuna jukumu kama kampuni pia kuitangaza Kenya. Nina furaha kwamba gavana anazungumza nasi kuhusu hilo,” alisema.

Quarcoo amesema Radio Africa iko tayari kushirikiana na wizara hiyo ili kuongeza idadi ya watalii.

“Kwa kila dola unayowekeza kwetu, tutatoa dola moja katika kampeni. Tunaona fursa kubwa katika ushirikiano na tutakuwa tukipendekeza mambo machache na mtatuongoza,” alihakikishia.

WAZIRI PENINAH MALONZA NA MKUU WA KITENGO CHA MAUDHUI PAUL ILADO
Image: ENOS TECHE

Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Radio Africa Group Martin Khafafa, Meneja wa Matukio Somoina Kimojino, Afisa Mkuu wa Masoko Caroline Mutoko na Mkuu wa Kitengo cha Maudhui Paul Ilado walioambatana na Quarcoo katika mkutano huo.

Malonza kwa upande mwingine aliambatana na maafisa wakuu kutoka Shirika la Huduma ya Wanyamapori la Kenya, Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya, Bodi ya Utalii ya Kenya, Bomas ya Kenya na Taasisi ya Utafiti wa Utalii ya Kenya.

Image: ENOS TECHE