Polisi wawakamata washukiwa 2 waliojifanya wapelelezi

Waliita polisi wakiwalazimisha washukiwa kutafuta njia ya kutoroka waliposikia gari la polisi likija.

Muhtasari
  • DCI ilisema kuwa washukiwa hao wawili walivamia nyumba moja katika ghorofa ya Elim Shepherd mwendo wa saa moja asubuhi
Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi Alhamisi walikamata washukiwa wawili ambao walikuwa wakijifanya kuwa maafisa wa polisi.

Walikamatwa baada ya kuvamia ghorofa moja eneo la Kihunguro Ruiru, Kaunti ya Kiambu wakidai kuwa wapelelezi.

Katika taarifa siku ya Ijumaa, DCI ilisema kuwa washukiwa hao wawili walivamia nyumba moja katika ghorofa ya Elim Shepherd mwendo wa saa moja asubuhi.

"Washukiwa walijitambulisha kama maafisa wa upelelezi katika kituo cha polisi cha Pangani," DCI alisema.

Wakaazi walitilia shaka na wakapiga kelele na kuwavutia maafisa kutoka kituo cha polisi cha Ruiru ambao walifika eneo la tukio.

Waliita polisi wakiwalazimisha washukiwa kutafuta njia ya kutoroka waliposikia gari la polisi likija.

"Majibu ya haraka ya maafisa wa Ruiru yaliwashangaza majambazi hao huku mmoja wao akijaribu kuruka kutoka ghorofa ya 3 hadi kutua kwenye ghorofa hiyo na kumjeruhi kichwa," DCI alisema.

Polisi walisema kuwa wahitimu wawili wa hivi majuzi wa Kiganjo waliwakabili washukiwa hao na mmoja wao akaanguka na kumjeruhi vibaya kichwani.