Watu watachizi!Ledama amtaka Sakaja kuondoa marufuku ya vilabu vyenye kelele

Alishutumiwa kwa kuwanyanyasa wafanyabiashara ambao alikuwa ameahidi kuwalinda wakati wa kampeni zake.

Muhtasari
  • Seneta wa Narok Ledama Olekina sasa ameangazia sakata hiyo na ana maoni kwamba hatua ya Sakaja haikushughulikiwa kwa kina
LEDAMA 2
LEDAMA 2

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja almaarufu Super Gavana amekuwa na wakati mgumu katika azma yake ya kuifanya Nairobi kuwa Jiji la utaratibu na hadhi.

Katika hali ya kushangaza, Sakaja amepata upinzani mkubwa kutoka kwa watu ambao awali walikuwa washirika wake wa kisiasa na hata kuunga mkono kuchaguliwa kwake kama gavana.

 

Hatua ya kwanza ya gavana wa Nairobi ilikuwa kufungwa kwa vilabu vilivyokuwa vikifanya kazi katika maeneo ya makazi ya Jiji la Nairobi.

Alishutumiwa kwa kuwanyanyasa wafanyabiashara ambao alikuwa ameahidi kuwalinda wakati wa kampeni zake.

Wabunge wake wa UDA walimgeukia katika hatua hiyo, wakitishia hatua ya kumfungulia mashtaka.

Seneta wa Narok Ledama Olekina sasa ameangazia sakata hiyo na ana maoni kwamba hatua ya Sakaja haikushughulikiwa kwa kina.

Olekina ana maoni kwamba kufungwa kwa vilabu kutawafanya Wakenya kuwa wazimu kwani watakosa mahali pa kupunguzia mafadhaiko.

Alibainisha kuwa kelele katika vilabu ndiyo tiba tosha ya mafadhaiko yote yanayotokana na waajiri na wenzi wa ndoa.

"Hivi karibuni Wakenya wataenda Gaga ... Sasa niambie ikiwa vilabu vyote vya NBI vimesimamishwa kucheza muziki unadhani watu watafanya nini na msongo wa mawazo - ukienda kazini bosi wako anakusisitiza - unarudi nyumbani mwenzi wako anakusisitiza haiya. @SakajaJohnson watu watachizi! Kelele ni dawa,"Alisema Olekina.