Manyora: Ruto, Raila wanapaswa kupatana kwa maslahi ya Wakenya

“Ninamwalika Ruto kutazama mambo haya kwa umakini zaidi kuliko anavyofanya,” Manyora alisema.

Muhtasari
  • Akizungumza siku ya Jumatatu, Manyora alisema viongozi hao wawili wanapaswa kurudiana kwa maslahi ya Wakenya
Star, KWA HISANI
Star, KWA HISANI
Image: Herman Manyora

Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Herman Manyora amesema kuwa Rais William Ruto anafaa kuwa kaka mkubwa kwa kufanya handshake na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

Akizungumza siku ya Jumatatu, Manyora alisema viongozi hao wawili wanapaswa kupatana kwa maslahi ya Wakenya.

"Ruto ana jukumu kubwa la kuwa kaka mkubwa kwa sababu ni yeye pekee anayeweza kunyoosha mkono wake kwa Raila. Haiwezi kutoka kwa Raila," Manyora alisema kwenye mahojiano na NTV.

Alisema kuwa Rais hawezi kufanya mengi Wakenya wanapokuwa mitaani.

“Ninamwalika Ruto kutazama mambo haya kwa umakini zaidi kuliko anavyofanya,” Manyora alisema.

"Iwapo mtu yeyote anashauri kuna chochote anachoweza kufanya wakati watu bado wako mitaani anamsingizia kwa sababu hakuna unachoweza kufanya na hakuna hata mmoja wao atakayeshinda ikiwa hawatazungumza."

Manyora alisema kuwa kanuni za Azimio haziwezi kubadilishwa kwa kutumia mamlaka ya serikali.

Hii ni baada ya Raila kufanya mikutano miwili ya kumpinga Ruto.

Raila alimtaka Ruto kukubali kwamba hakushinda uchaguzi wa urais wa Agosti 2022.

Raila alisema Rais Ruto anafaa kuondoka Ikulu....“Kubali kwamba ulishindwa kwenye uchaguzi, ondoka Ikulu ili Baba aingie,” akasema.

"Tunasema ukweli, hatutaki vita, na hatutaki vitisho. Tuna haki zetu kama Wakenya, na haziwezi kupokonywa na mwewe, Wakenya wanastahili kiongozi waliyemchagua."