EACC yawakamata wanachama 6 wa bodi ya huduma ya maji kwa madai ya ufisadi

"Sita hao ni pamoja na Maafisa wanne wa Bodi ya Huduma za Maji katika Bonde la Ufa

Muhtasari
  • Tume ilisema washukiwa hao wanazuiliwa katika afisi ya Mkoa wa Bungoma wakisubiri kufikishwa mahakamani
Makao yatume ya maadlili na kupambana na ufisadi
EACC Makao yatume ya maadlili na kupambana na ufisadi
Image: MAKTABA

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi Jumatano iliwakamata wanachama sita wa Bodi ya Huduma ya Maji ya Rift Valley kwa madai ya ufisadi.

Tume hiyo ilisema katika taarifa yake tuhuma zinazowakabili sita hao kuhusiana na utoaji wa kandarasi kinyume na utaratibu wa ujenzi wa Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Malaba, Ujenzi wa Usambazaji wa Maji kwa gharama ya Sh600 milioni.

"Sita hao ni pamoja na Maafisa wanne wa Bodi ya Huduma za Maji katika Bonde la Ufa waliokamatwa katika maeneo ya Nakuru na Eldoret na maafisa wawili kutoka Bodi ya Huduma ya Maji ya Ziwa Victoria Kaskazini waliokamatwa kwa wakati mmoja katika kaunti za Nandi na Kakamega," EACC ilisema.

Tume ilisema washukiwa hao wanazuiliwa katika afisi ya Mkoa wa Bungoma wakisubiri kufikishwa mahakamani katika Mahakama ya Kupambana na Ufisadi ya Bungoma siku ya Alhamisi.

Watashtakiwa kwa makosa mbalimbali yakiwamo ya kutofuata kwa makusudi sheria.