NSSF: Wakenya kukatwa Ksh 2000 badala ya Ksh 200 kila mwezi - Mahakama ya rufaa

Jopo hilo la majaji watatu lilidumisha uamuzi wa mwaka 2013 uliotaka kiwango hicho kuongezwa kutoka 200 hadi 2000.

Muhtasari

• Mahakama iliwataka waajiri wote kukumbatia hilo na kuongeza kiwango cha wafanyikazi wao kwa asilimia 6 ili kuchangia fedha za NSSF.

NSSF kuongezwa kwa asilimia 6.
NSSF kuongezwa kwa asilimia 6.
Image: Maktaba

Mahakama sasa imedumisha uamuzi wa mwaka 2013 uliotaka mchango wa fedha za NSSF kwa kila Mkenya mwenye ajira kupandishwa kutoka kiwango cha shilingi 200 kwa mwezi hado shilingi 2000 kwa mwezi.

Majaji watatu wa mahakama ya rufaa walidumisha uamuzi huo wa 2013 na kusema kwamba kila mwajiri ataongeza kiwango chake kwa asilimia 6, ikiwa ni kutoka shilingi mia mbili hadi elfu mbili kutokana na mapato yake ya kila mwezi.

Majaji wa Mahakama ya Rufaa Hannah Okwengu, Mohamed Warsame na John Mativo waliamua kuwa Sheria ya NSSF ya 2013, iliyotaka kuongeza michango ya kila mwezi kutoka Shilingi 200 hadi Shilingi 2,000, ni halali.

Uamuzi huu unatoka miezi michache tu baada ya rais William Ruto kusisitiza kuwa kuna haja kwa Wakenya kuongeza kiwango hicho kwa manufaa yao wenyewe.

Ruto alisema kuwa pesa hizo ambao zinafaa kuongezwa zitahakikisha kwamba Mkenya anapofikisha miaka 60 ya kustaafu, angalau anapata fedha za maana za kumsindikiza kwenda nyumbani kuliko jinsi ambavyo ilivyo sasa hivi Mkenya analipa shilingi 200 kila mwezi na iifika muda wa kustaafu anapata fedha za NSSF ambazo si za maana kuonesha bidi yake ya miaka Zaidi ya 30 kama mwajiri.

“Watu wengi kwenye orodha ya NSSF wanalipa Shilingi 200, ni mshangao tumetoka tu kupata uamuzi kutoka kortini wiki moja iliyopita kwamba ni makosa sisi kuongeza kutoka Shilingi 200, sijui tunafanya nini. Je, tunaishi katika nchi moja?" Ruto alisema basi.