Mwanahabari Francis Gachuri apata kazi katika Wizara ya mambo ya ndani

Pia atasimamia njia zote za mawasiliano za ndani na nje ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Uratibu wa Kitaifa.

Muhtasari
  • Waziri wa Mambo ya Ndani Kindiki Kithure alimteua Gachuri kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika wizara hiyo
MWANAHABARI FRANCIS GACHURI
Image: KWA HISANI

Mhariri wa kisiasa wa Royal Media Service Francis Gachuri anatazamiwa kujiunga na Wizara ya Mambo ya Ndani kufuatia uteuzi wake mpya.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kindiki Kithure alimteua Gachuri kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano katika wizara hiyo.

Katika mahojiano ya kipekee na The Star, Gachuri alithibitisha uteuzi huo na kusema atatoa taarifa kufuatia habari hiyo.

“Nitatoa taarifa muda si mrefu,” alisema.

Katika jukumu lake jipya, Gachuri atakuwa na jukumu la kuunda, kutoa na kutathmini shughuli za mawasiliano zitakazopelekea uwekaji nafasi na kukuza uaminifu ndani ya Wizara.

Pia atasimamia njia zote za mawasiliano za ndani na nje ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Uratibu wa Kitaifa.