Gharama ya maisha kupanda hata zaidi huku bei ya mafuta ikiongezeka kwa shilingi 2

EPRA ilitangaza bei hiyo mpyaa itatumika Kuanzia tarehe,15, Machi

Muhtasari

•EPRA ilisema bei ya dizeli na mafuta taa itabaki vile vile.

Petrol
Petrol

Gharama ya maisha inatarajiwa kupanda hata zaidi baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Kawi na Petroli (EPRA)  nchini kutangaza nyongeza kwa bei ya petroli kwa shilingi mbili kwa lita. 

Katika bei za hivi punde, EPRA hata hivyo ilitangaza kuwa bei ya dizeli na mafutaa taa haitabadilika na yatauzwa kwa ksh.162 na ksh. 145 mtawalia mjini Nairobi.

Kwa upande mwingine, bei ya petroli itapanda hadi ksh 179.20 kwa lita moja jijini Nairobi.

"Bei ya petroli imepandishwa ili kuwezesha ruzuku kuwekewa mafuta ya dizeli huku ruzuku ya ksh 23.49, ikisalia kwa mafuta taa," ilisema EPRA .

Bei ya mafuta ilipanda marudufu punde tu rais William Ruto alipotwaa mamlaka ya uongozi na kuondoa ruzuku.

Hili lilifanyika baada ya Ruto kuondoa ruzuku iliyokuwa imewekwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta akidai kuwa hatua hiyo iliwafaidi watu wachache matajiri.

Rais Ruto alishusha bei ya mbolea huku akisema kuwa ni muhimu kutoa ruzuku kwa uzalishaji kuliko matumizi.