Hatutaki udikteta-Wanga,Babu Owino wavunja kimya baada ya wanasiasa na waandamanaji wa Azimio kukamatwa

Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo pamoja na wabunge Amina Mnyazi na Ken Chonga wanazuiliwa.

Muhtasari
  • Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, amewakashifu polisi kwa kugeuza maandamano ya amani kuwa ya vurugu.
wakati wa maandamano mnamo Machi 20, 2023.
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wakati wa maandamano mnamo Machi 20, 2023.
Image: EZEKIEL AMINGA

Baada ya Polisi kuwakamata viongozi wa upinzani na waandamanaji kwa kushiriki maandamano dhidi ya serikali katika mji mkuu, Nairobi, wabunge wa mrengo wa zimio wamejitokeza na kukemea tukio hilo.

Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo pamoja na wabunge Amina Mnyazi na Ken Chonga wanazuiliwa.

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, amewakashifu polisi kwa kugeuza maandamano ya amani kuwa ya vurugu.

"Tunataka kuwashukuru maafisa wa polisi kwa kutumia pesa za walipa ushuru kununua vitoa machozi, kwanza ya leo ni tamu sana, mnunue zaidi," Owino alisema.

Zaidi ya hayo, Babu aliwakashifu polisi kwa madai ya kumuua mwandamanaji mmoja katika eneo la Jacaranda na wengine wawili katika eneo la Kibra.

Aliongeza kuwa hakuna kinachoweza kuwazuia kuendelea na maandamano.

"Leo ni mazoezi tu, tutafanya hivi kila wiki. Hatutarudi nyuma kwa sababu ya vitoa machozi na risasi," alisema.

Huu Gladys Wannga akizungumzia kukamatwa kwa wanasiasa na waandamanaji hao alisema kwamba watapambana vyema,huku akimwambia Rais Wakenya hawtaki udiktet.

"Rais nataka kukwambia kwamba hatutaki udikteta nchini, tutapambana na kukimbizana tuko hapa hatubanduki,"Wanga alisema.