Ledama Olekina: Jitayarisheni kwa siku 14 za maandamano

Maandamano yaligeuka kuwa ya ghasia katika majiji ya Nairobi na Kisumu

Muhtasari

• Kinara wa Azimio Raila Odinga,alitangaza maandamano ya kitaifa kupinga uongozi wa rais Ruto na kumshinikiza afungue sava za IEBC pamoja na kupunguza gharama ya juu ya maisha.

LEDAMA 2
LEDAMA 2

Seneta wa Narok Ledama Olekina sasa amewatahadharisha Wakenya wawe tayari kwa siku 14 na nne za maandamano katika jiji la Nairobi.

Katika chapisho la Twitter, Olekina amedai kuwa maandamano hayo yatafanywa hadi wakati sava za IEBC zitafunguliwa .Amedai pia kuwa watawacha kuandamana pale rais Ruto atakaposhusha gharama ya maisha na kusitisha  mpango wa kuajiri maafisa wapya wa IEBC bila kuwahusisha.

Kinara wa Azimio Raila Odinga, alitangaza maandamano ya kitaifa kupinga uongozi wa rais Ruto na kumshinikiza afungue sava za IEBC pamoja na kupunguza gharama ya maisha ya juu.

Maandamano hayo yalianza siku ya Jumatatu katika sehemu tofauti zaidi jijini Nairobi. Kumeshuhudiwa ghasia katika maeneo ya Nairobi na Kisumu polisi wakilazimika kukabiliana na waandamanaji kwa kuwarushia vitoa machozi na kuwatawanyisha.

Baadhi ya viongozi wa Azimio la umoja wamekamatwa wakiwemo Mbunge wa Unguja,Opiyo Wandayi na seneta wa Kilifi Stewart Madzayo. Imeripotiwa pia kuwa baadhi ya vigogo hao wa Azimio wamezuiliwa kuondoka manyumbani kwao na polisi.

Viongozi hao wa Azimio wamemshutumu rais Ruto kwa kile walichodai ni udikteta. Walisema kuwa maandamano yaikuwa ya amani ila polisi ndio walianza kuzua vurugu.