Wakili Miguna amsuta DCI kwa uamuzi wake kuhusu kifo cha Jeff

Wakili Miguna amekashifu DCI kuhusu uamuzi wake kuhusu kifo cha Jeff Mwathi.

Muhtasari
  • Ripoti za awali zilizotolewa na DCI zilionyesha kuwa Jeff aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa nje ya nyumba.
Image: TWITTER// MIGUNA MIGUNA

Wakili Miguna Miguna amevunja ukimya wake baada ya maafisa wa DCI kusema kuwa Jeff Mwathi alifariki kutokana na kujitoa uhai.

Ripoti za awali zilizotolewa na DCI zilionyesha kuwa Jeff aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa nje ya nyumba.

Aidha, taarifa hizo pia zilionyesha kuwa haiwezekani kwa mtu yeyote wa umri kupita kwenye grili za madirisha nyumbani kwa DJ Faxto.

Ripoti ya hivi punde iliyotolewa na DCI ilifichua kuwa Jeff alijitoa uhai kwa kuruka kutoka kwa nyumba ya Faxto kupitia dirishani.

Hii imezua taharuki miongoni mwa Wakenya.

Wakili Miguna amekashifu DCI kuhusu uamuzi wake kuhusu kifo cha Jeff Mwathi. Kulingana na Miguna, Jeff Mwathi aliuawa kabla ya kutupwa nje ya nyumba.

"Kuhusu uchunguzi wa MAUAJI ya Geoffrey Mwathi, maoni yangu ni kwamba @DCI_Kenya wachunguzi wameonyesha kutokuwa na uwezo na/au maelewano ya kimaadili. Mwathi aliuawa na kutupwa nje ya jengo. Hadithi nyingine yoyote ni hogwash."

Katika taarifa iliyotolewa na DCI, ilisema kuwa DJ Faxto hakuhusishwa na kifo cha Jeff kwa sababu hawakuwa na ushahidi.