Mchekeshaji Eric Omondi aachiliwa kwa bondi

Wote walikana mashtaka ya kushiriki katika mkusanyiko usio halali kinyume na Kifungu cha 79 cha Kanuni ya Adhabu.

Muhtasari
  • Pia alipinga ombi la upande wa mashtaka kutaka washtakiwa wasijihusishe tena na shughuli hiyo.
  • Omondi akiandamana na Maxwell Bunde, Austin Oduor, Zephaniah Ouma na Sylvester Omondi walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Nixon Onyango.
alikamatwa akiongoza maandamano mjini Kisumu Aprili 26, 2023
Eric Omondi alikamatwa akiongoza maandamano mjini Kisumu Aprili 26, 2023
Image: FAITH MATET

Mcheshi Eric Omondi na wenzake wanne wameachiliwa kwa bondi ya Sh20,000 kila mmoja, na dhamana ya pesa taslimu mbadala ya Sh 10,000 kila mmoja.

Omondi akiandamana na Maxwell Bunde, Austin Oduor, Zephaniah Ouma na Sylvester Omondi walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Nixon Onyango.

Wote walikana mashtaka ya kushiriki katika mkusanyiko usio halali kinyume na Kifungu cha 79 cha Kanuni ya Adhabu.

Hata hivyo, mwendesha mashtaka Onanda Tony alibainisha kuwa washtakiwa wanapaswa kuachiliwa kwa dhamana kwa sababu baadhi yao hawakuwa wakazi wa jiji la Kisumu.

Aidha Onanda aliiomba mahakama hiyo pia iwaamuru washitakiwa hao kutoshiriki tena shughuli hizo kinyume na sheria hata kesi itakapoendelea.

Haya yalipingwa na wakili mshtakiwa Kowino Omondi akisema wateja wake wanapaswa kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu.

Alibainisha kuwa watatu kati ya washtakiwa walikuwa wanafunzi na walikaa Kisumu kwa hivyo hawakuwa hatarini, akiongeza kuwa Omondi anatoka eneo hilo lakini anakaa Nairobi pekee.

"Hii sio msingi wa kuwanyima wateja wetu dhamana ya pesa taslimu kwa sababu sio hatari".

Pia alipinga ombi la upande wa mashtaka kutaka washtakiwa wasijihusishe tena na shughuli hiyo.

"Hii itakuwa inakiuka haki za kikatiba za mteja wangu, suala hili bado halijaamuliwa na mahakama ikiwa ana hatia au la," Kowino alisema.

 

Hata hivyo, Hakimu alisema hawezi kulikubali ombi la upande wa mashtaka kwa sababu hiyo itakuwa inakiuka haki za washtakiwa.

Alisema shauri hilo litatajwa Mei 8 ili kuthibitisha iwapo taarifa hizo zimetolewa na pande zote mbili.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Juni 5, 2023.