Mahakama yawakubalia wapelelezi kuchunguza akaunti za benki za Odero

Polisi pia wameruhusiwa kuchunguza laini saba za M-Pesa za Odero.

Muhtasari

• Akaunti hizo ni za kutoka benki tano ambazo ni pamoja na benki ya Cooperative, Equity, NCBA, HFC na KCB Bank.

• Maafisa wa upelelezi wa DCI wameruhusiwa kuchunguza akaunti tatu zinazoendeshwa na Mchungaji Ezekiel Odero kuhusu madai ya kutakatisha fedha.

mchungaji Ezekiel Odero
mchungaji Ezekiel Odero
Image: Facebook

Maafisa wa upelelezi wa DCI wameruhusiwa kuchunguza akaunti tatu zinazoendeshwa na Mchungaji Ezekiel Odero kuhusu madai ya kutakatisha fedha.

Mahakama ya Milimani ilikubali maagizo yaliyotakwa na inspekta mkuu Martin Munene ambaye aliomba mahakama ichunguze akaunti za Odero anayeshukiwa kuwa katika mpango wa ufujaji wa pesa.

“Ni muhimu na inafaa kumpa mwombaji hati ya kuchunguza vitabu vya akaunti za benki na huduma za fedha kwa njia ya simu ili kumpa mamlaka afisa kupata vitabu vinavyohusiana na namba kadhaa za akaunti,” taarifa za mahakama zilisoma.

Akaunti hizo ni za benki ya Cooperative, Equity, NCBA, HFC na benki ya KCB ambazo zinamilikiwaa na mchungaji Eekiel na kanisa lake la New Life International.

Polisi pia wameruhusiwa kuchunguza laini saba za M-Pesa za Odero.

DCI inaeleza kuwa wanamtaka afisa anayayeongoza uchunguzi kukagua, kuchambua ripoti na kutaka kukabidhiwa nakala zilizoidhinishwa za nyaraka za kufungua akaunti, taarifa za akaunti ya benki, watia saini wa akaunti, RTGS (mwepesi) kwa kipindi cha kati ya Januari 14, 2017; hadi Aprili 30, 2023, na hati nyingine yoyote inayofaa ambayo inaweza kumsaidia kukamilisha uchunguzi kuhusu kesi inayoshukiwa ya utakatishaji fedha.

"Kutoa agizo la kuwalazimisha wahusika wa 1,3, 4, 5 na 6 kumteua mtu au watu walioidhinishwa kurekodi taarifa, kutoa kwa afisa wa uchunguzi," DCI asema katika ripoti za mahakama.

Benki ya Cooperative, Equity, KCB na benki ya HFC pamoja na Safaricom ndio wahusika wa 1, 3, 4 na 6 katika kesi hiyo.