Watu wawili wamefariki kwenye ajali iliyohushisha magari manne mjini Migori

Walioshuhudia ajali hio walisema kuwa breki za lori hio zilikatika na kupoteza mwelekeo

Muhtasari

• Kamanda wa polisi wa gatuzi ndogo ya Suna Magharibi Elizabeth Wakuloba alisema bado wanakusanya data kutoka kwa hospitali zilizo karibu kuhusu vifo zaidi.

• Breki zaa lori hilo zilikatika lilipokaribia mji wa Migori kutoka eneo la Kakrao kabla ya kuyagonga magari na wapiti njia.

Image: STAR

Breki zaa lori hilo zilikatika lilipokaribia mji wa Migori kutoka eneo la Kakrao kabla ya kuyagonga magari na wapiti njia.

Watazamaji walisema lori hilo lilikuwa limebeba mchanga.

Afisa mkuu wa polisi kaunti ya Migori Mark Wanjala alisema mmoja alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini na wengine 11 wako katika hali mahututi.

Aliongeza kuwa meingine alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Migori.

"Majeraha yalikuwa makubwa lakini siwezi kujua kina ya majeraha hayo," Wanjala alisema.

“Tumepoteza mmoja huku wengine wakiwa hospitalini. Tumewakimbiza majeruhi hospitalini.”

Kamanda wa polisi wa gatuzi ndogo ya Suna Magharibi Elizabeth Wakuloba alisema bado wanakusanya data kutoka kwa hospitali zilizo karibu kuhusu vifo zaidi.

"Kufikia sasa tumethibitisha kifo kimoja katika Hospitali ya Rufaa ya Migori. Tuko eneo hilo na polisi wameanzisha uchunguzi," Wakuloba alisema.

Wakuloba aliongeza kuwa bado wanakusanya takwimu kutoka vituo vingine vya afya.

Sehemu hio hio ilishuhudia ajali mbaya Aprili 8 ambapo takriban watu sita walifariki baada ya dereva wa lori kupoteza udhibiti na kugonga pikipiki na magari yaliyokuwa yameegeshwa kando ya barabara.

Image: STAR