Maribe akanusha kuhusika kwa vyovyote katika mauaji ya Monica Kimani

Alieleza kwamba alimfahamu siku ambayo alisoma habari kuhusu kifo chake.

Muhtasari
  • Alifikishwa mahakamani kupitia mienendo yake siku ambayo kosa hilo linadaiwa kutokea.

Jacque Maribe mshukiwa wa mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani amejitetea akisema hakuwa na nia ya kutaka auawe.

Maribe alimweleza hakimu Grace Nzioka kwamba hamfahamu Monica.

Alieleza kwamba alimfahamu siku ambayo alisoma habari kuhusu kifo chake.

"Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumsikia na kuona picha yake. Sikuwahi kukutana naye wala sikufanya mazungumzo yoyote na Jowie kuhusiana na Monica," alisema.

Alifikishwa mahakamani kupitia mienendo yake siku ambayo kosa hilo linadaiwa kutokea.

Alisema mnamo Septemba 19, 2018, aliondoka kwenye makazi yake huko Royal Park kwa kazi. Mchumba wake wa wakati huo Jowie alimpeleka hadi RMS mwendo wa saa nane asubuhi.

Mahakama ilisikia kwamba alikuwa RMS siku nzima hadi 9.30 pm.

Maribe alisema alipokuwa akiondoka, alikutana na msafara wa aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko ambaye alikuwa ameratibiwa kuhudhuria mahojiano na Jeff Koinannge.

Saa 10 jioni, Maribe aliondoka kuelekea Q Lounge, mkahawa ulio mkabala na Citizen TV.

Alitazama mahojiano hayo kwenye simu yake hadi ilipoisha chaji.

Saa 11.30 jioni, alisema mwenzake Monica Kiragu alifika kwenye chumba cha mapumziko cha Q na kumwarifu kuwa Jowie alikuwa akimtafuta.

“Kwa kuwa simu yangu ilikuwa imezimwa alinitafuta kwa kutumia namba ya Monica,” alisema.

Maribe alisema baadaye alimpigia simu Jowie na kumwarifu kwamba alikuwa akienda klabu ya 4040 na msafara mmoja wa Anita Thumbi na Sonko.

Awali Jowie akiwa mbele yan hakimu Grace alidai kwamba alipata majeraa baada ya kujipiga risasi,kutokana na ujumbe aliouona kwa simu ya Maribe.

Pia alidai kwamba hakumfahamu Monica bali alifahamu ndugu yake, ambaye walikuwa wanasoma pamoja.