Mahakama yatupilia mbali ombi la Ezekiel la kurejeshewa akaunti za benki

Jaji wa Mahakama Kuu Olga Sewe alisema ombi hilo ni potofu na haliwezi kutekelezeka.

Muhtasari

•  Jaji Sawe Alisema ataepuka kutoa maoni yake kuhusu usahihi na uhalali wa maagizo yaliyotolewa na Mahakama ya Nairobi wiki jana.

• Odero aliwasilisha ombi lake katika Mahakama Kuu ya Mombasa mnamo Mei 3 akiomba amri ya serikali kufungia zaidi ya akaunti 15 za kibinafsi na za kanisa.

Mchungaji Ezekiel Odero mahakamani.
Mchungaji Ezekiel Odero mahakamani.

Mahakama kuu ya Mombasa imetupilia mbali ombi la Mchungaji Ezekiel Odero la kutaka akaunti zake zaidi ya 15 za benki zisifungwe.

Jaji wa Mahakama Kuu Olga Sewe alisema ombi hilo ni potofu na haliwezi kutekelezeka.

Alisema ataepuka kutoa maoni yake kuhusu usahihi na uhalali wa maagizo yaliyotolewa na Mahakama ya Nairobi wiki jana.

Mahakama Kuu pia ilitupilia mbali ombi la maagizo yaliyotaka leseni ya TV yake kerejeshwa, ikisema walalamishi walipaswa kutumia njia zote za kisheria na Mamlaka ya Mawasiliano kabla ya kufika mahakamani.

Odero aliwasilisha ombi lake katika Mahakama Kuu ya Mombasa mnamo Mei 3 akiomba amri ya serikali kufungia zaidi ya akaunti 15 za kibinafsi na za kanisa.