Mwanamke akamatwa kwa kumlazimisha mwanawe,4, kula kinyesi chake

"Kama jirani, huwezi kuona mtoto akiteswa mara kwa mara halafu ukanyamaza."

Muhtasari
  • Hii ilikuwa baada ya video kuibuka mtandaoni, ikimuonyesha mshukiwa akimlazimisha mtoto huyo kula kinyesi chake siku ya Jumatatu.
Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi nchini Uganda wamemkamata mwanamke mmoja baada ya kudaiwa kumlazimisha mtoto wake wa kambo wa miaka 4 kula kinyesi chake.

Hii ilikuwa baada ya video kuibuka mtandaoni, ikimuonyesha mshukiwa akimlazimisha mtoto huyo kula kinyesi chake siku ya Jumatatu.

Msemaji wa Polisi wa Uganda Enanga Fred alithibitisha kukamatwa kwa mtoto huyo na kusema timu yake inakwenda kumpeleka mtoto huyo kwenye makazi ya ulinzi na kuhakikisha anapata matibabu.

'Yuko chini ya ulinzi wetu katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jinja na tumefungua kesi ya kuteswa na kunyanyaswa kwa watoto. Tunataka kumshukuru jirani kwa kutufahamisha kwa sababu ni kitendo cha ujasiri," Enanga alisema.

"Kama jirani, huwezi kuona mtoto akiteswa mara kwa mara halafu ukanyamaza."