Waziri wa elimu Ezekiel Machogu kuzindua kufunguliwa kwa tovuti ya KUCCPS

Haya yanajiri baada ya serikali kuzindua muundo mpya wa ufadhili wa vyuo vikuu.

Muhtasari

• Watahiniwa wa mtihani wa mwaka 2022 basi watahitajika kuanza kuchagua kozi zao na taasisi wanazotaka kwenye tovuti.

• Vyuo vikuu viliagizwa kuwasilisha kwa Kuccps gharama za vitengo vyao ili kuwawezesha watahiniwa kuchagua kozi na taasisi wanazoweza kumudu.

WAZIRI WA ELIMU EZEKIEL MACHOGU
Image: ANDREW KASUKU

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kuongoza kufunguliwa kwa shughuli ya kuteuliwa kwa watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa shule ya upili (KCSE) wa mwaka wa 2022 katika vyuo vikuu.

Waziri huyo ataongoza kufunguliwa rasmi kwa tovuti hio ya KUCCPS katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Watahiniwa wa mtihani waa mwaka 2022 basi watahitajika kuanza kuchagua kozi zao na taasisi wanazotaka kwenye tovuti.

Haya yanajiri baada ya serikali kuzindua muundo mpya wa ufadhili wa vyuo vikuu.

Vyuo vikuu viliagizwa kuwasilisha kwa Kuccps gharama za vitengo vyao ili kuwawezesha watahiniwa kuchagua kozi na taasisi wanazoweza kumudu.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuagiza taasisi za elimu ya juu kuweka hadharani gharama ya vitengo vyao kabla ya wanafunzi kutuma maombi ya kujiunga na chou hizi.

Chini ya mtindo huo mpya uliozinduliwa na Rais William Ruto, serikali italipa tu karo za masomo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu vya umma peke yake.

Huku wale ambao watachagua vyuo vikuu vya kibinafsi, ambavyo vinachukuliwa kuwa ghali, wanatarajiwa kulipa karo zao wenyewe kupitia mikopo ya serikali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Hapo awali, vyuo vikuu vilifadhiliwa kupitia Ufadhili wa Vyuo Vikuu kwa kutumia viwango tofauti vya gharama ambavyo vilitekelezwa kuanzia mwaka wa 2015.