Nairobi: Raha yageuka karaha majambazi wakivamia baa usiku na kuwaibia wapiga sherehe

Ripoti ilisema majambazi hao walikuwa wamebeba gunia chakavu migongoni wakijifanya 'chokoraa' kabla ya kuingia kwenye klabu hiyo na kutoa bunduki.

Muhtasari

• Kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya DCI, Majangili hao watatu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

• Awali walijifanya kama wazururaji wa akili isiyo na afya wakiwa wamebeba magunia migongoni mwao

Majangili wavamia klabu cha usiku na kuwaibia wanywaji.
Majangili wavamia klabu cha usiku na kuwaibia wanywaji.
Image: Maktaba

Matukio ya raha katika sehemu moja ya kustarehe jijini Nairobi eneo la Ruaraka yaligeuka kuwa ya karaha baada ya genge la majambazi kuvizia klabu hiyo na kuwaibia wanywaji kwa mtutu wa bunduki.

Kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya DCI, Majangili hao watatu waliokuwa wamejihami kwa bunduki awali walijifanya kama wazururaji wa akili isiyo na afya wakiwa wamebeba magunia migongoni mwao, kabla ya kuingia katika baa ya Reke Marie kutafuta ‘riziki’ yao.

Wakati huo wote, wale wapiga sherehe ambao hawakuwa na wasiwasi na waliendelea kuoza tezi zao za umio bila kuadhibiwa huku wakiburudika kwa vinywaji baridi, hadi mmoja wa wale waliodhaniwa kuwa ni wazimu akatoa bunduki na kuamuru kila mtu alale chini!, DCI walisimulia.

“Kila mtu lala chini!’’ aliwaamuru majambazi hao huku klabu nzima ikinyamaza ghafla. Mmoja wa washereheshaji ambaye alionekana kuzidiwa na ulevi alijibu “kwani wewe ni nani?...” huku mwenzi wake akimtania “nyamaza! ni majangili!” sehemu hiyo ya DCI ilisoma.

Kisha majambazi hao walikuwa na wakati rahisi wakipora mifuko yao kwa simu za rununu, pesa taslimu na vitu vingine vya thamani.

Walevi wengine ambao hawakuwa wanajua kilichokuwa kikiendelea walizidi kunong’ona baina ya ulevi wao wakitema cheche kali kwa majambazi hao.

Hili liliwafanya majambazi hao kufyatua risasi mbili hewani na kuwavutia maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria, ambao mara moja walikimbilia eneo la tukio. Hata hivyo, wakati wa kuwasili kwao majambazi walikuwa wametoweka gizani, DCI ilisema huku ikidhibitisha kwamba msako dhidi yao umeng’oa nanga.