KATIBA IFUATWE KUBUNI SHERIA

Seneta wa Busia Omtatah afika mahakamani kupinga mswada wa fedha

Mawakili wakiri kwamba mswada huo si wa kikatiba

Muhtasari

•Mwanaharakati Okiya Omtatah na wengine wanne wamewasili mahakamani ili kupinga mswada wa fedha  unaopendekezwa 2023.

•Kipengele 76 hutishia haki za wanajamii kiuchumi, kwa kiwango ambacho iwapo utafanywa kuwa sheria,waajiriwa watapunguziwa 3% katika mishahara yao, huku nayo 3% ya waajiri wakihitajika punguza idadi ya wafanyakazi wao ambao huenda wakachangia gharama kubwa katika biashara zao.

Mwanaharakati Okiya Omtatah na wengine wanne wamewasili mahakamani ili kupinga mswada wa fedha  unaopendekezwa 2023.

Kulingana na dua lao, wanapinga kwamba mswada huo utakuwa unazidhalilisha haki ya binadamu za kiuchumi kisha kuchangia gharama kubwa katika baadhi ya bidhaa iwapo mswada huo utafanywa kuwa sheria.

“Inasubiri kusikilizwa na mahakama itakuwa radhi kutoa amri ya kusitisha mjadala kulingana na vipengele 28,30,33,36 na 76 vya mswada wa fedha mwaka wa 2023.” Akisoma karatasi za mahakama.

Pia wameisihi mahakama kutoa amri ya muda kumkataza spika wa bunge la kitaifa kukubaliana na pendekezo la rais kuukubalisha mswada wa fedha 2023 ambao unahusu vipengele vilivyotajwa.

“Kipengele 76 hutishia haki za wanajamii kiuchumi, kwa kiwango ambacho iwapo utafanywa kuwa sheria,waajiriwa watapunguziwa 3% katika mishahara yao, huku nayo 3% ya waajiri wakihitajika punguza idadi ya wafanyakazi wao ambao huenda wakachangia gharama kubwa katika biashara zao.” Walijitetea.

Katika majibizano yao, mswada huo ni ulaghai ambao  utawawekea vikwazo jinsi ya kuchagua mipango yao katika ujenzi wa nyumba au namna ya kutumia mali yao.

Kulingana na watano hao, kipengele cha 76 cha mswada pia kinatishia uhuru wa kumiliki mali ukipendekeza kuwa wafanyakazi wa umma lazima washiriki katika ushuru uliowekwa kama njia ya kudhihirisha uhalisia wa umiliki wa  mali yao.

“Iwapo itakuwa sheria, kipengele 76 kinatishia walipaushuru katika idara rasmi za kikazi hatua ya kiutawala isiyofaa kukinzana na sheria huku ikipendekeza kila mmoja kupata nyumba kwa mpango wanaouita ufadhili wa nyumba.” Akisoma karatasi za mahakama.