logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali kutenga shilingi bilioni 10 kwa Hustler Fund katika bajeti ya 2023-2024

Serikali imetenga Sh10 bilioni kwa Hustler Fund katika bajeti ya 2023/2024.

image
na Davis Ojiambo

Habari15 June 2023 - 13:23

Muhtasari


  • • Gavana huyo wa zamani wa Benki Kuu ya Kenya alisema serikali imeshuhudia ukuaji wa ajabu wa miamala ambao unafikia miamala shilingi milioni 43.5.
  • •Rais William Ruto alizindua bidhaa ya tatu ya Hustler Fund Juni 1.
Waziri wa Hazina Njuguna Ndung'u akiwa Bungeni kwa ajili ya kutangaza makadirio ya Bajeti ya 2022-2023 mnamo Juni15, 2023.

Serikali ya imetenga shilingi bilioni 10 kwa Hustler Fund katika bajeti ya 2023/2024.

Waziri wa Hazina ya taifa Njuguna Ndung'u alisema kuwa fedha hizo za ziada zitasaidia juhudi za serikali katika kuwezesha ujasiriamali nchini.

Alisema tangu kuzinduliwa kwa bidhaa ya kwanza, serikali imewekeza shilingi bilioni 11  ili kutoa riba nafuu kwa asilimia nane kwa mwaka.

Ndung'u alisema kufikia sasa Wakenya milioni 16, ambapo milioni 7.1 ni wateja wa kuchukua mikopo tena, wamepata hazina hiyo.

“Mpaka sasa shilingi bilioni 30.8 zimekopwa kutoka kwenye Hustler Fund, pamoja na kukopa, mfuko huu umeundwa ili kuhamasisha uwekaji akiba, leo shiling bilioni 1.5 zimeokolewa kuwa akiba ya lazima huku shilingi milioni 17 zikiwa kwenye akiba ya hiari. " alisema.

Gavana huyo wa zamani wa Benki Kuu ya Kenya alisema serikali imeshuhudia ukuaji wa ajabu wa miamala ambao unafikia miamala shilingi milioni 43.5.

Rais William Ruto alizindua bidhaa ya tatu ya Hustler Fund Juni 1.

Mkopo wa kikundi cha Hustler Fund ulizinduliwa wakati wa sherehe za 60 za Madaraka Day tarehe Mosi mwenzi Juni.

"Nina furaha kutangaza kwamba wakati wa sherehe za leo, nitazindua mpango ambao unalenga kuwezesha watu kupata ufadhili kupitia vikundi," Ruto alisema.

"Sasa ni heshima na furaha yangu kutambulisha na kuzindua rasmi bidhaa ya Hustler Fund, Hustler Group Loan. Nina hakika kwamba hii itakuwa habari njema sana kwa rafiki yangu mzuri Shiko kutoka Ruaka," aliongeza.

Ruto alieleza kuwa ili kukuza ujumuishi wa Wakenya wote, Hustler Fund itapeleka vikundi kama vile vyama na saccos ili kuondokana na kutengwa na vizuizi vya kushiriki katika mikopo, akiba, hifadhi ya jamii, bima ya afya na huduma zingine za kijamii na kiuchumi.

Mpango huo wa mikopo ya bei nafuu umeundwa mahususi kusaidia wafanyabiashara wadogo nchini.

Hustler Fund inajumuisha bidhaa nne: Mikopo ya watu binafsi, Biashara ndogo, SME na mikopo ya kuanzisha biashara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved