Jambazi aliyekuwa akiwahangaisha wakazi wa Nairobi akamatwa na DCI

DCI ilisema kuwa Otieno ana kesi inayosubiri mahakamani kwa kosa sawia na kwamba alikuwa nje kwa bondi.

Muhtasari
  • DCI pia ilisema kuwa oparesheni ya kuwakamata washirika wake na kuwafikisha mahakamani iko mbioni.
Image: DCI/TWITTER

Jambazi maarufu ambaye amekuwa akiwahangaisha wakazi wa Kayole na viunga vyake amenaswa na maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Mshukiwa huyo aliyetambulika kama Luis Otieno almaarufu Lui Borura Nyaoiri, anaaminika kuwa kiongozi wa genge ambalo limehusika katika visa vya uvunjaji wa nyumba na wizi katika eneo hilo.

Kulingana na taarifa kutoka kwa DCI, Otieno alikamatwa siku ya Jumanne alipokuwa akiendesha gari la Mazda Demio lililokuwa limewekwa bamba la nambari ghushi.

Gari hilo lilikuwa limeripotiwa kuibwa na mmiliki wake ambaye alikuwa amepoteza thamani ya maelfu ya pesa kwa genge hilo.

Baada ya kupekua nyumba ya Otieno, maafisa hao walipata saa za aina mbalimbali za mkono, bunduki za kale zilizoning'inia ukutani, simu za rununu, kompyuta kibao, diski za sauti, spika za masikioni, roli tisa za vitu vinavyoshukiwa kuwa na athari za kisaikolojia miongoni mwa vitu vingine.

Bidhaa hizo zinaaminika kuibwa kutoka kwa nyumba mbalimbali katika Kaunti Ndogo ya Kayole.

DCI ilisema kuwa Otieno ana kesi inayosubiri mahakamani kwa kosa sawia na kwamba alikuwa nje kwa bondi.

DCI pia ilisema kuwa oparesheni ya kuwakamata washirika wake na kuwafikisha mahakamani iko mbioni.

"Jambazi maarufu anayeshukiwa kuwa kiongozi wa genge maarufu ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa jiji, amekamatwa na majambazi wa DCI mkoani Nairobi.

Luis Otieno almaarufu Lui Borura Nyaoiri ambaye ana kesi inayosubiri kortini alikamatwa kufuatia visa vya uvunjaji nyumba na wizi ulioripotiwa katika Kaunti Ndogo ya Kayole, ambapo waathiriwa wamepoteza thamani ya maelfu ya pesa.

Jambazi huyo ambaye alikamatwa akiendesha gari la usajili la Mazda Demio namba KDM 790K ambalo awali lilikuwa limefungwa namba tofauti KDD 790K, aliwaongoza maafisa hao hadi nyumbani kwake ambapo baada ya kupekuliwa, saa za mkononi za aina mbalimbali, bunduki za kale zilizoning'inia kwenye ukuta, simu za mkononi. , kompyuta kibao, flash disks, viridi, vipokea sauti vya masikioni, Rombo tisa (9) za dutu inayoshukiwa kuwa dutu ya kisaikolojia miongoni mwa vitu vingine zilipatikana.

Operesheni ya kuwakamata washirika wake na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria iko mbioni."