Ndugu wawili wadaiwa kumuua mpenzi wa mama yao Embu

Mmoja wa wanaume hao alikamatwa baadaye huku mwingine akitoroka baada ya tukio la Jumatatu, Septemba 4.

Muhtasari
  • Peter Mwangi aliaga dunia baada ya kupigwa na wanaume wawili waliomshtumu kwa kujaribu kuchukua familia yao.
crime scene
crime scene

Katika kijiji cha Kiambere, Kaunti ya Embu, mwanamume mwenye umri wa miaka 45 aliuawa katika boma ambalo alikuwa ameenda kumuona anayedaiwa kuwa mpenzi wake.

Peter Mwangi aliaga dunia baada ya kupigwa na wanaume wawili waliomshtumu kwa kujaribu kuchukua familia yao.

Polisi walisema marehemu alikuwa ameenda kukutana na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni mama wa wanaume hao wenye umri wa miaka 20 na 23 wakati mapigano yalipozuka.

Wanaume hao waliamuru marehemu kuondoka nyumbani kwa mama yao na kusababisha mapigano ambayo yaligeuka kuwa mbaya.

Mmoja wa wanaume hao alikamatwa baadaye huku mwingine akitoroka baada ya tukio la Jumatatu, Septemba 4.

Polisi walisema msako wa kumtafuta mshukiwa mwingine unaendelea.

Mwili huo ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.