Raila sio mwanachama wa ODM-Mchambuzi wa kisiasa Maliba adai

Anasema kuwa kulingana na kanuni za vyama vya kisiasa, Odinga hawezi kuwa mwanachama wa ODM na Azimio kwa wakati mmoja.

Muhtasari
  • Kulingana na mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa, wabunge walioathirika wanapaswa kupumzika na wasisumbuliwe na uamuzi unaotolewa na chama.

Mchanganuzi wa kisiasa Arnold Maliba anadai uamuzi wa Chama cha ODM kuwatimua wanachama wake watano ambao walionekana kukosa uaminifu ni batili.

Kulingana na Maliba, hatua ya kinidhamu ambayo iliidhinishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) haiwezi kusimama kwa vile Raila Odinga, ambaye aliongoza mkutano huo, ni mwanachama wa Chama cha Muungano cha Azimio La Umoja One Kenya.

Anasema kuwa kulingana na kanuni za vyama vya kisiasa, Odinga hawezi kuwa mwanachama wa ODM na Azimio kwa wakati mmoja.

“Uamuzi na hata kauli iliyotolewa na John Mbadi ni batili kwa sababu mgeni aliongoza kamati ya nidhamu. Raila ni mgeni katika ODM. Raila si mwanachama wa ODM. Raila na Martha Karua ni wanachama wa Azimio na wamejidhihirisha hadharani kama watu waliowania Azimio ambayo kwa hakika ni chama,” alisema Maliba kwenye mahojiano na NTV.

Kulingana na mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa, wabunge walioathirika wanapaswa kupumzika na wasisumbuliwe na uamuzi unaotolewa na chama.

“Kwa hiyo wabunge waliofukuzwa wafurahi kwa sababu mgeni wa chama aliongoza kamati ya nidhamu. Msajili wa vyama vya siasa Anne Nderitu anapaswa kujitokeza wazi na atuambie ikiwa kifungu cha 14 kinafaa haswa ambapo hakuna mtu anayepaswa kuwa wa vyama viwili vya kisiasa," mtaalamu huyo wa kisiasa alisema.

Aliongeza: “Raila alikimbia Azimio. Bado anaomba seva zifunguliwe akisema Azimio alishinda. Kwa hiyo, alikaa katika nafasi gani. Huyu ni mgeni anayeketi katika mkutano wa ODM ili kuwaadhibu wanachama wa ODM.”