Takriban asilimia 38 ya Wakenya wanaamini kuwa serikali ya Rais William Ruto imetimiza ahadi zake za kampeni.
Katika utafiti wa Tifa, 38% ya Wakenya wanasema wanaamini kuwa serikali ya Ruto imefanya vyema katika kutimiza ahadi zake za kampeni ikilinganishwa na 31% mwezi Juni.
Asilimia 49 ya wanaounga mkono serikali wanaamini kuwa serikali ya Ruto imefanya vyema katika kutimiza ahadi zake za kampeni.
Hata hivyo, ni asilimia 29 tu ya waliohojiwa wanaounga mkono upinzani wanaamini kuwa uimetimiza ahadi yake.
Pia, 32% ya waliohojiwa bila mfungamano wa kisiasa wanaamini Ruto ametimiza ahadi yake.
Kulingana na Tifa, wahojiwa 1,007 walihojiwa kati ya Septemba 8-10, 2023.
Sampuli hiyo ilisambazwa katika kanda 9 zikiwemo Central Rift, Pwani, Mashariki ya Chini, Mt Kenya, Nairobi, Kaskazini, Nyanza, South Rift na Magharibi.
Mahojiano hayo yalifanyika kupitia mahojiano ya simu na wahojiwa ambao mawasiliano yao yalikusanywa kupitia ana kwa ana hapo awali.