• Kuwaelekeza wageni waliopotea na ambao wanatafuta ramani si jambo gumu kwa wana Zanzibar.
Katika moja ya Makala ya kustaajabisha ambayo yamefanywa na BBC, kisiwa cha Zanzibar ni moja ya sehemu ambayo ukarimu ni wa viwango vya kupitiliza.
Kwa mujibu wa Makala hayo kwa njia ya video, mtu yeyote katika kisiwa cha Zanzibar akipoteza pesa au mali yake, basi moja kwa moja ta ngazo linawekwa redioni hadi pale kitu hicho kitakapopatikana.
“Aliibiwa mgeni na baadhi ya watu ambao sio waaminifu, mwizi huyo alifuatiliwa na kikapatikana kitu chake na akatafutwa na mwenyewe akapewa. Ndio maana mpaka kesho watu huko nje ya Zanzibar wanahamasishana huku ni sehemu salama,” mzee mmoja mkaazi wa Zanzibar alisema.
Kwa mujibu wa Makala hayo, Zanzibar ndicho kisiwa au sehemu ambayo inachukuliwa kuwa salama Zaidi duniani kwa ukarimu ambao wageni haswa watalii wanaooneshwa na wenyeji.
Kuwaelekeza wageni waliopotea na ambao wanatafuta ramani si jambo gumu kwa wana Zanzibar.
“Unajua Zanzibar ni tamaduni zetu na mila zetu, hata mimi toka niko mdogo tulifundishwa kuwa wapole na wakarimu kwa watu tunaokutana nao. Na haswa haswa watu ambao hatuwajui. Kwa sababu huwezi kujua yule mtu usiyemjua ni nani, na hilo limekuwa jambo la kipekee linalofaya Zanzibar kuwa kivutio kwa watalii,” Nahya Zahir, mkaazi wa Zanzibar alisema.
Mzee Khatibu Mwinyi, mkazi wa Zanzibar aliiambia BBC kwamba ukarimu ni historia ya Zanzibar tangu kitambo akisema kuwa Imani ndio imewajenga wengi kuwa na ukarimu huo uliopitiliza.