•Alihojiwa na baadaye kukabidhiwa kwa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi kwa maelezo zaidi.
•Mwanamume huyo alitarajiwa kortini ambapo polisi walipanga kuomba muda zaidi wa kumshikilia huku wakichunguza tukio hilo.
Kulishuhudiwa kizazaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati mwanamume raia wa Ghana aliyekuwa safarini kwenda Dubai alipokamatwa akiwa amebeba risasi tatu.
Polisi walisema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 33, alinaswa katika eneo la uchunguzi wa uwanja wa ndege alipokuwa akipanga kuondoka kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways.
Raia huyu alipatikana na risasi hizo kwenye kituo hicho ambapo ni kinyume cha sheria katika tukio la Jumatano, polisi walisema.
Polisi walisema alinyimwa kuondoka, akahojiwa na baadaye kukabidhiwa kwa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi kwa maelezo zaidi.
Nia yake ya kumiliki risasi hizo na kujaribu kusafiri nazo hadi Dubai bado haijafichuliwa.
Mwanaume huyu alibainika kuwa alikuwa amekaa jijini Nairobi kwa muda, polisi wakibaini kuwa wanashuku kuwa alitoka na risasi hizo nchini.
"Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha risasi hizo," polisi walisema.
Mwanamume huyo alitarajiwa kortini ambapo polisi walipanga kuomba muda zaidi wa kumshikilia huku wakichunguza tukio hilo.
Risasi ni miongoni mwa vitu vilivyopigwa marufuku kwenye ndege. Abiria wanatakiwa kuzisalimisha kwa mashirika ya ndege na kutoa hati za kuzimiliki.