logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kisii: Jamaa aua mke na watoto wa ndugu yake kufuatia mzozo wa kinyumbani

Aliwaua mke wa ndugu yake pamoja na watoto wawili wenye miaka 4 na 3 mtawalia.

image
na Davis Ojiambo

Habari15 November 2023 - 09:22

Muhtasari


  • • Vikosi vya usalama vya eneo hilo vilihamasishwa kumzuia mhalifu huyo kabla hajaondoka mkoani humo, juhudi ambazo zilizaa matunda jana usiku.
Mshukiwa wa mauaji.

Makachero wa DCI katika kaunti ya Kisii wamemdaka mwanamume mmoja anayeshukiwa kuwaua watoto na mke wa ndugu yake.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo ilichapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za DCI, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27, Alex Ayata Migosi kutoka kijiji cha Mesaria kaunti ya Kisii alikamatwa baada ya kuchimba mitini kufuatia tukio hilo la unyama.

“Alex Ayata Migosi ambaye alikimbilia mafichoni baada ya mauaji hayo kunaswa jana usiku, saa chache baada ya kisa cha Jumanne tarehe 14 eneo la Kegogi katika kaunti ndogo ya Marani, Kisii,” sehemu ya taarifa ya DCI ilisom.

DCI walisema kwamba muda mfupi kabla ya tukio hilo, majirani waliripotiwa kushuhudia makabiliano makali kati ya mshukiwa wa mauaji na kakake Patrick Omuga kuhusu suala ambalo halijathibitishwa.

Katika azimio la kuchukiza la kusuluhisha matokeo, Ayata aliingia kisiri ndani ya nyumba ya ndugu huyo akiwa na panga, akiwaua kwa uchungu wale watatu waliokuwa wanyonge kwa hofu na shutuma za ujirani.

Vikosi vya usalama vya eneo hilo vilihamasishwa kumzuia mhalifu huyo kabla hajaondoka mkoani humo, juhudi ambazo zilizaa matunda jana usiku.

Kwa sasa anashughulikiwa ili afikishwe mahakamani.

Aliwaua mke wa ndugu yake pamoja na watoto wawili wenye miaka 4 na 3 mtawalia.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved