Mamake mwanamke wa mafuta ya 17Bn asema hajawahi onana na bintiye kwa miaka 5

“Ni ukweli ninamkosa sana binti yangu, lakini ninataka aje kuniona, lakini kila mara ananiambia kwamba yuko bize,” mama huyo wa miaka 71 aliambia NTV.

Muhtasari

• “Huwa tu tunaonana kupitia kwa video na nimekubali hilo kwa sababu kama ako sawa pia mimi ninafarijika,” aliongeza.

Mama na binti wa dizeli ya bilioni 17
Mama na binti wa dizeli ya bilioni 17
Image: Screengrab//NTVKenya

Mamake mwanamke wa miaka 55 anayedai kuwa mmiliki halali wa shehena ya mafuta dizeli yenye thamani ya shilingi bilioni 17 ambayo imeshikiliwa katika bandari ya Mombasa kwa zaidi ya mwezi sasa amesema kwamba hakuwahi kujua kwamba bintiye ni tajiri kiasi hicho.

Kufuatia unganganyaji mkubwa ambao umemzingira Ann Njeri anayedai kuwa mmiliki wa mafuta hayo, runinga ya NTV ilifanya ziara ya kipekee nyumbani kwa mama yake Githunguri kaunti ya Kiambu na kwa kustaajabu, mamake Pauline Njoroge alisema kwamba kando na kutojua utajiri wa bintiye, pia hajawahi kutana na bintiye kwa kipindi cha miaka 5.

“Ni ukweli ninamkosa sana binti yangu, lakini ninataka aje kuniona, lakini kila mara ananiambia kwamba yuko bize,” mama huyo wa miaka 71 aliambia NTV.

“Huwa tu tunaonana kupitia kwa video na nimekubali hilo kwa sababu kama ako sawa pia mimi ninafarijika,” aliongeza.

Mama huyo alisema kwamba kama kuna kitu kinachomsumbua akili ni kupata taarifa kupitia vyombo vya habari wiki jana kuhusu kutoweka kwa bintiye, akisema kwamba hakuwahi kujua kwamba ni mfanyibiashara mkubwa hivyo wa bidhaa za kawi.

“Kama kuna kitu kinanisumbua huwa ninamuambia kupitia simu, na kila mara ninapomuomba usaidizi huwa haraka kunisadia,” alisema.

Ann Njoroge aligonga vichwa vya habari wiki jana na sasa ametakiwa kujitokeza mbele ya kamati ya bunge kuhusu kawi Jumatano wiki Kesho ili kutoa mwanga Zaidi kuhusu sakata hilo la mafuta ya dizeli ambayo yanazozaniwa baina yake na kampuni nyingine na ambayo yamekwama bandarini kwa Zaidi ya mwezi sasa.