Kiambu: Afisa wa GSU atorokea benkini baada ya kumuibia mteja wa M-Pesa (video)

Maskini GSU alipoona hali imekuwa tete, alilazimika kukimbia kwa wenzake wanaoweka ulinzi katika tawi la benki moja na kujitoma ndani ya benki hiyo kwa kishindo.

Muhtasari

• Jambazi huyo alimpokonya elfu 50 hizo na kabla ya kuondoka zake, mteja yule alipiga kamsa iliyowafungua maskio na macho watu katika mji huo.

Bunduki
Bunduki
Image: Andrew Kasuku

Afisa wa kitengo cha GUS katika mji wa Ruiru kaunti ya Kiambu ana bahati kuwa hai baada ya jaribio lake la ujambazi kutibuka.

Inaarifiwa kwamba afisa huyo aliyekuwa amejihami kwa bunduki aina ya bastola akimvizia mtu mmoja aliyekuwa ametoa pesa taslimu kiasi cha laki mbili katika tawi la benki moja katika mji huo kabla ya kueleka katika duka la M-Pesa kufanay miamala ya kuziweka ndani ya simu yake.

Afisa huyo alimfuata nyatu nyatu kutoka benki hadi katika duka la M-Pesa na wakati mtrja huyo aliondoa pesa hizo kumkabidhi mhudumu wa M-Pesa ili kumtilia ndani ya simu yake, alimnyooshea bunduki na kumtaka kumkabidhi kila kitu.

Kwa bahati nzuri, mteja huyo alikuwa ametoa shilingi elfu 50 mfukoni na ndizo alizokuwa anahakiki hesabu kabla ya kumkabidhi mhudumu wa M-Pesa.

 Jambazi huyo alimpokonya elfu 50 hizo na kabla ya kuondoka zake, mteja yule alipiga kamsa iliyowafungua maskio na macho watu katika mji huo.

Watu walimfuata mbio jambazi huyo pasi na kujua kwamba alikuwa ni afisa wa polisi.

Maskini GSU alipoona hali imekuwa tete, alilazimika kukimbia kwa wenzake wanaoweka ulinzi katika tawi la benki moja na kujitoma ndani ya benki hiyo kwa kishindo, jambo lililowafanya maafisa wengine kutuliza umma uliojawa na mungali.

Baadae ndio walikuja kubaini kwamba mshukiwa huyo Nahashon Ekidor, alikuwa ni afisa wa GSU kitengo cha Recce katika mji wa Ruiru.

Walimweka chini ya ulinzi na taarifa zilisema kwamba atafikishwa mahakamani mapema Jumatatu wiki kesho kwa shtaka la kufanya ujambazi.

KSh 54,100 zilipatikana katika ghasia hizo. Kuthibitisha kutokea, Benki ya Equity ilithibitisha kuwa hali ya kawaida ilirejeshwa.