logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sasa uchumi wa Kenya uko imara, tumethibiti uchumi wetu! - Ruto adai kwa ujasiri (video)

Alisema Kenya itaanza kulipa madeni yake mwezi Desemba.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 November 2023 - 11:00

Muhtasari


  • • Rais alikuwa akizungumza katika Kaunti ya Kirinyaga ambapo aliagiza ujenzi wa barabara ya Sagana-Kathaka-Thiguku.
  • • “Hata mliona wiki iliyopita, IMF walitupea dola milioni 950. Tunaanza kulipa madeni ile imesumbua nchi yetu kwanzia hii Disemba,” alisema rais.
Rais William Samoei Ruto

Licha ya idadi kubwa ya Wakenya kuhisi kwamba taifa linaelekea pabaya kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha ya kuporomoka kwa uchumi, rais William Ruto kwa upande wake anadai kwamba uchumi wa Kenya umeimarika pakubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kiongozi huyo wa taifa alikuwa akizungumza katika Kaunti ya Kirinyaga ambapo aliagiza ujenzi wa barabara ya Sagana-Kathaka-Thiguku.

Alisema kwamba chini ya utawala wake, uchumi wa Kenya umaimarika pakubwa na mikakati ambayo ameiweka imewezesha Kenya kuthibiti uchumi wake katika mkondo salama kwa siku zijazo.

“Sasa uchumi wa Kenya uko imara, tumeweza kuthibiti uchumi wetu,” kiongozi wa taifa alisema.

Vile vile, Ruto aliweza kuzungumzia suala la madeni ya taifa ambayo tunadaiwa na mashirika mbali mbali ya kitaifa, akizungumzia pia rundo la deni jingine ambalo shirika la kimataifa la kutoa mikopo, IMF lilisaini na Kenya mwishoni mwa juma lililopita.

Ruto alitetea mkopo huo mpya akisema kwamba utaliwezesha taifa kujiimarisha kiuchumi hata Zaidi na kufichua kwamba kuanzia mwezi Desemba Kenya itaanza kulipa duru ya kwanza ya madeni yake ya tangu miaka takribani 10 iliyopita.

Hata mliona wiki iliyopita, IMF walitupea dola milioni 950. Tunaanza kulipa madeni ile imesumbua nchi yetu kwanzia hii Disemba,” alisema rais.

Hata hivyo, Ruto alikiri kwamba anafahamu fika jinsi Wakenya wamelemewa na mzigo mzito wa kodi lakiji akasema kwamba hakuna njia nyingine ya kulinasua taifa kutokana na madeni, bali ni kuashughulikia madeni hayo kwa mara moja ya kuyamaliza kabla ya Wakenya kuanza kufurahia unafuu wa maisha bila madeni miaka ijayo.

“Mambo ni magumu lakini lazima tuyashughulikie. Njia ya kubadilisha Kenya ndio hii,” Ruto aliongeza.

Wakati huo huo, kiongozi wa taifa alidokeza Wakenya kufurahia unafuu japo kwa kiduchu kuanzia mwezi kesho akifichua kwamba bei za mafuta zitaanza kushuka.

“Mmeona mwezi huu bei zimeanza kupungua. Mwezi ujao zitashuka hata zaidi,” akasema Rais.

Kuhusu mambo mazuri yajayo, Ruto alihakikishia Wakenya kwamba kuanzia mwakani, mambo yatanoga hata Zaidi na miradi iliyosimama kufufuliwa, kwa tafsiri kwamba kuteseka ni kwa muda tu!

"Mambo yatakuwa mazuri mwaka ujao kwa kuwa tumekabiliana na vikwazo vikali ambavyo tulipata. Nawatangazia kuwa nina imani kuanzia mwakani miradi yote ya maendeleo iliyokuwa imekwama itafufuliwa kwa sababu tumeweza kusimamia uchumi wetu,” aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved