logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila achukizwa na hatua ya jaji mkuu Martha Koome kuitikia wito wa rais Ruto ikuluni (video)

Odinga alisema kwamba mazungumzo hayo yangefanyika nje ya ikulu.

image
na Davis Ojiambo

Habari22 January 2024 - 13:27

Muhtasari


  • • Hata hivyo, Jumatatu asubuhi, Martha Koome alikubali wito wa Ruto katika ikulu, jambo ambalo lilionekana kumuudhi Odinga.
  • • Mwanasiasa huyo alidai kuwa mtendaji huyo anashikilia mfumo wa mahakama, kulingana na video iliyoshirikiwa na ODM.
Jaji mkuu Martha Koome amekubaliana na Ruto kwamba uchaguzi na uamuzi viliwezesha na Mungu

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameonesha kukerwa kwake na hatua ya jaji mkuu Martha Koome kuitikia wito wa rais Ruto katika ikulu ya Nairobi, siku chache baada ya kutupiana maneno kuhusu ufisadi katika idara ya mahakama.

Baada ya Rais Ruto kudai kwamba idara ya mahakama imegubikwa na ufisadi, jaji Koome alikashifu madai hayo vikali na kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliingilia kati na kumtaka Ruto kuheshimu idara hiyo huru.

Hata hivyo, baadae Ruto alionekana kulegeza msimamo wake na kusema kwamba angetafuta mwafaka wa kulitatua suala hilo na idara ya mahakama, jambo ambalo lilimfanya Odinga kuonya vikali jaji  mkuu dhidi ya kukubali mwito.

Hata hivyo, Jumatatu asubuhi, Martha Koome alikubali wito wa Ruto katika ikulu, jambo ambalo lilionekana kumuudhi Odinga.

Mwanasiasa huyo alidai kuwa mtendaji huyo anashikilia mfumo wa mahakama, kulingana na video iliyoshirikiwa na ODM.

"CJ ameenda kwa mkutano na rais katika ikulu. Hii, kwa maoni yetu, ni hatua ya kutowajibika. Ikiwa ilipaswa kuwa na mazungumzo, basi yafanyike kwa msingi usio na upande. “

“Ikulu ni mkuu wa mtendaji, kiti cha mtendaji. Hapo ndipo rais anapoishi. Iwapo kutakuwa na mazungumzo kuhusu masuala ya utawala, basi yanapaswa kuwa ya upande wowote. Hii ina maana kwamba mfumo wa mahakama unahujumiwa na watendaji. Idara ya mahakama inazuiliwa na mtendaji huyo," alidai Raila.

Alisema kuwa upinzani umetoa onyo dhidi ya mkutano unaoendelea hivi sasa.

"Tuliionya Idara ya Mahakama kutolala na mtendaji huyo. Haya ni maendeleo ya bahati mbaya. Tunataka kutumaini kwamba wajumbe wa mahakama hawatahujumiwa. Tunawataka majaji waendelee kuwa imara na kufanya kazi yao kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi yetu," aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved