logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa stima leo, Alhamisi

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Aprili 4.

image
na SAMUEL MAINA

Habari04 April 2024 - 04:35

Muhtasari


  • •KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la South C zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Aprili 4.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Machakos,Migori, Nyeri, Embu, Kirinyaga, Kiambu, Busia, na Bomet.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la South C zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za  maeneo ya mji wa Machakos, Athi River na  Kangundo Road, Joska, Malaa  katika kaunti ya Machakos zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Gogo na Rapogi katika kaunti ya Migori zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa nane alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Blueline, Munyu, Kimahuri, Kiawambogo, Kianguru, Nyagatugu, Muthinga, Gichira, Kangaita na Wanjerere zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya soko ya Kianjiru na na Mururi na afisi ya gavana katika kaunti ya Kirinyaga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kivwe, Makengi, Kevote, Ena, Kithimu, na Rukira katika kaunti ya Embu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za maeneo ya Thika Green na Gitingiri katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa saba mchana.

Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Nambale DC, Lugulu, Madende, Namahindi, na Mungatsi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi  na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chesilyot na Kaplong katika kaunti ya Bomet pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved