KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Mei 21.
Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Baringo,Trans Nzoia, Nyeri, Kisii, Nyandarua na Kiambu.
Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Prisons, OJ, BTI, Kidfarmaco na mji wa Kikuyu zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Kitalale na Kinyoro katika kaunti ya Trans Nzoia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Weru na Murungaru katika kaunti ya Nyandarua zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Giakaibei na Naromoru zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Mogotio Equator na Muya katika kaunti ya Baringo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za mji wa Kisii katika kaunti ya Kisii zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja jioni.