Polisi Mbooni Mashariki, Kaunti ya Makueni wanamshikilia mwanamke mwenye umri wa miaka 32 nayedaiwa kumuua mumewe mwenye umri wa miaka 82.
Kulingana na Albanus Mutula, msaidizi wa chifu wa eneo hilo, wanandoa hao walitofautiana kuhusu Ksh.3,000 huku marehemu akimshutumu mkewe mchanga kwa kuiba pesa hizo.
Syombua Musau anadaiwa kumpiga mumewe kwa mawe mgongoni na kumuua papo hapo.
Mwanamke huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mbumbuni akisubiri kusomewa mashitaka.
Mwili wa mzee huyo ulipelekwa katika chumba cha maiti cha Tawa.
Msimamizi huyo aliwataka wakazi kutafuta njia mwafaka za kutatua tofauti zao bila kuchukua hatua za kurudi nyuma.
uy67