logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Ijumaa- KPLC

baadhi ya maeneo ya kaunti nne yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni

image
na Davis Ojiambo

Habari31 May 2024 - 05:57

Muhtasari


  • •Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
    •Kaunti ambazo zitaathirika ni Makueni, West Pokot, Nyeri,na Mombasa.

Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Mei 31.

Katika taarifa ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kunatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Kampuni ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na  moja jioni.Kaunti ambazo zitaathirika ni Makueni, Nyeri,Mombasa na West Pokot .

Katika kaunti ya Makueni, sehemu kadhaa kama Sultan Town, Sultan Police, Holy Ghost Schools, Kalimbini, Ngokomi, Kwothithu, Kiongwani, Kima, Kiu, Salama, Kautandini, Malili, Enzai, Nunguni, Kilungu, Kavatanzou, Mitini, Kyambekezitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chorong'i C/Fact, Kiamwathi Market,katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Mjini Mombasa, sehemu ambazo zitaathirika ni  Shule ya Upili ya Shimo Latewa, Mama Ngina Girls, Flamingo Hotel, Serena Residences, Mtwapa Town, Mtoondoni, Mtepeteni na wateja walio karibu.

Maeneo ya Pokot Magharibi ambayo yataathiriwa ni pamoja na Siyoi, Kaibos, Paraiywa, Kabichbich, Kipat, Kapsait, Kaptabuk, Kokwoplekwa, Kapsangar na wateja walio karibu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved