logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Nyeri, Busia, Kiambu, na Mombasa.

image
na SAMUEL MAINA

Habari06 June 2024 - 04:33

Muhtasari


  • •KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Nyeri, Busia, Kiambu, na Mombasa.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Juni 6.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Nyeri, Busia, Kiambu, na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Garden Estate na baadhi ya viunga vyake vitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Makutano, Kapenguria, Murkwijit, Safari Hotel, Kamatira, na Kesogon katika kaunti ya West Pokot zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tano asubuhi.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kamatogu, Honi Resort, Mwireri, Jersey Farm, na Aberdare County Club katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Busia, baadhi ya sehemu za maeneo ya Butula na Bumutiru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi  na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za Tola, Bob Harris, Ngoingwa, Metro, TIBS, na Compuera katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Msumarini, Vipingo na Junju katika kaunti ya Mombasa pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved