Jamaa atiwa mbaroni kwa kujifanya wanahabari maarufu ili kuwalaghai Wakenya mashuhuri

Mshukiwa amekuwa akijifanya wanahabari maarufu ili kuomba manufaa ya kifedha kutoka kwa waathiriwa

Muhtasari

•Mshukiwa alikamatwa katika mtaa wa Zambezi na vifaa vya mawasiliano ambavyo anadaiwa kutumia katika uhalifu vilipatikana.

•Mtuhumiwa alidai kuwa ana Diploma ya Uandishi wa Habari kutoka taasisi maarufu ya habari nchini, wapelelezi wamesema.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: HISANI

Jamaa mmoja anayedaiwa kuwaigiza watangazaji maarufu wa vyombo vya habari kwa lengo la kuwalaghai Wakenya mashuhuri ametiwa mbaroni.

Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyetambulishwa alikamatwa katika mtaa wa Zambezi, eneo la Kikuyu, kaunti ya Kiambu na vifaa vya mawasiliano ambavyo anadaiwa kutumia katika uhalifu vilipatikana.

Kulingana na ripoti ya DCI, mshukiwa ambaye amekuwa akifanya kazi ya ulaghai kwa muda mrefu amekuwa akijifanya wafanyikazi maarufu wa vyombo vya habari ili kuomba manufaa ya kifedha kutoka kwa waathiriwa ambao hawana ufahamu..

Katika upotovu huo uliaoanza mwaka wa 2023, mshukiwa amekuwa akijifananisha na mwanahabari na mtangazaji wa redio Eric Latiff wa Spice FM ya Standard Group, akiwafikia wageni walioalikwa na mwanahabari huyo katika kipindi chake cha Situation Room.

Wakati katika sura hiyo, mshukiwa (ambaye lazima awe mfuasi sugu wa vipindi vyote vinavyoendeshwa na mlalamikaji) amekuwa akituma ujumbe wa ‘asante’ kwa wageni walio na hali nzuri baada ya kila shoo, lakini kama mwanzo tu kabla ya kujiingiza kwenye kamari zake za kimbinu.

Waathiriwa walengwa ambao walipoteza maelfu kwa muumini wa utajiri wa haraka anayedai kuwa Latiff akihitaji "kakitu nimekwama mahali" ni pamoja na Katibu Mkuu, mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa, mkurugenzi wa cheo cha juu katika KPLC, afisa katika Mitumba Consortium Association ya Kenya miongoni mwa nyingine,” DCI ilisema kwenye ripoti Jumatano.

Baada ya kukamatwa, mtuhumiwa huyo alidai kuwa ana Diploma ya Uandishi wa Habari kutoka taasisi maarufu ya habari nchini, wapelelezi wamesema.

Pia alidai kuwa hapo awali alifanya kazi na redio ya kidini.

"Ushahidi muhimu ikiwa ni pamoja na SIM kadi zilizotumiwa kutuma ujumbe kwa waathiriwa waliolengwa na kupokea pesa zilizoombwa zilipatikana kwake, na tangu wakati huo zimewasilishwa kwa Maabara ya Uchunguzi wa Kidijitali kwa uchunguzi," ripoti hiyo ilisema.

Maafisa wa upelelezi sasa wamepewa wiki moja kukamilisha uchunguzi kabla ya kumshtaki mshukiwa mahakamani.