Mwanamke asakanywa baada ya kumdunga mpenzi wake wa zamani kisu

Kisa hicho kilitokea katika eneo la Mihang'o huko Njiru,kaunti ndogo ya Kayole mnamo Aprili 22,2023.

Muhtasari

•Maafisa wa DCI wanamtafuta Mary Mwende ambaye ni mshukiwa wa kesi ya kujaribu kuua katika eneo la Mihang'o huko Njiru,kaunti ndogo ya kayole.

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Mwanamke mmoja anayefahamika kama Mary Mwende Kimwalu  yupo mawindoni na maafisa wa usalama baada ya tuhuma za kujaribu kuua.

Maafisa wa upelelezi wa DCI eneo la Kayole,kaunti ya Nairobi wapo katika harakati za kumsakanya huku wakiomba maelezo kuhusu aliko Mary Mwende Kimwalu,35 ambaye ni mshukiwa wa kesi ya kujaribu kuua katika eneo la Mihang'o huko Njiru,kaunti ndogo ya Kayole mnamo Aprili 22,2023.

Kupitia chapisho kwenye ukurasa wa Facebook,Mary Mwende aliripotiwa kumdunga mpenziwe wa zamani mara tatu kifuani kwa kutumia kisu cha jikoni,baada ya kusambaratisha mapenzi yao ya wakati mmoja.

Baada ya shambulio hilo baya,Mary alipotea isifahamike aliko huku akifuta ishara zote za kupatikana na hatia.Si hivo tu,kwani pia mwanamke huyo alikata  mawasiliano yake na familia yake hadi marafiki zake.

"Idara ya uhamiaji inathibitisha kwamba hajaondoka nchini,na hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi yake Mei 13,2024 inatumika.Rekodi za mshukiwa aliyeshikiliwa katika ofisi ya kitaifa ya usajili zinaonyesha  kuwa anatoka Ikutha , Kitui ya kati,eneo ndogo la Kyoani..." Taarifa kutoka maafisa wa DCI iliripoti.