Wakenya wameombwa kujitokeza kusaidia kuokoa maisha ya hakimu mkuu Monica Kivuti kufuatia tukio la kupigwa risasi katika mahakama ya Makadara.
Monica, kwa sasa anaendelea kupigania maisha yake baada ya kunusurika kuuawa kwa kupigwa risasi na afisa mkuu wa polisi anayejulikana kama Samson Kipruto.Afisa huyo alikuwepo mahakamani wakati wa kesi dhidi ya mkewe,alighadhabishwa na hatua ya hakimu Kivuti kufutilia mbali dhamana ya mkewe.
Kulingana na ripoti ya polisi, mke wa Kipruto alishtakiwa kwa kujipatia KSh 2.9 milioni kwa njia ya udanganyifu.
Aliyekuwa makamu wa rais wa chama cha sheria cha kenya[LSK] Carolyne Kamende aliwaomba wakenya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Monica,kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook,mnamo Alhamisi,Juni 13 2024.
Kwa sasa,hakimu amelazwa katika hospitali ya Metropolitan Buruburu na anahitaji damu kwa haraka.
"Tunamwombea Monica Kivuti na maofisa waliojeruhiwa. Mungu bado yuko nanyi kwa kila hatua na tunaamini mtapata uponyaji.Tufanye hivi watu wema." Carolyne Kamende aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook baada ya kuweka picha iliyoekwa maandishi ya kusaidia kuchangia damu.