Waziri Alfred Mutua amtembelea polisi aliyepoteza mikono wakati wa maandamano ya Jumanne

Mutua alitembelea hospitali ya Nairobi West ambapo Inspekta Mkuu David Karuri Maina amelazwa.

Muhtasari
  • Mutua alitembelea hospitali ya Nairobi West ambapo Inspekta Mkuu David Karuri Maina amelazwa.
Waziri Alfred Mutua amtembelea polisi aliyepoteza mikono wakati wa maandamano ya Jumanne
Image: ALFRED MUTUA/ X

Waziri wa Utalii Alfred Mutua Alhamisi alimtembelea afisa wa polisi aliyepoteza mikono yake yote miwili katika eneo la CBD Nairobi wakati wa maandamano ya Jumanne ya kupinga Mswada wa Fedha, 2024.

Mutua alitembelea hospitali ya Nairobi West ambapo Inspekta Mkuu David Karuri Maina amelazwa.

"Ziara yangu inaangazia athari kubwa ya machafuko ya hivi majuzi kwa watu wanaohusika na jamii pana, ikisisitiza hitaji la uvumilivu, umoja na ustahimilivu katika nyakati zenye changamoto," alisema kwenye X.

Huku akithibitisha haki ya Wakenya kuandamana, waziri huyo alionya dhidi ya maandamano yanayoendeshwa na harakati na propaganda tu.

Maina na afisa mwingine walijeruhiwa vibaya baada ya kitoa machozi kuwalipua jijini Nairobi.

Haya yanajiri kufuatia kushindwa kwa Maina kutotoa mkebe uliolipuliwa wakati wa maandamano yaliyomgharimu mikono miwili.

Afisa wa pili wa kike alipata majeraha mabaya kifuani baada ya kitoa machozi kuwalipua.

Maina alikuwa miongoni mwa maafisa waliotumwa kuwadhibiti waandamanaji alipolipua kitoa machozi nje ya Kencom mkabala na International Life House.