Worldcoin kurejelea shughuli zao nchini Kenya baada ya uchunguzi dhidi yao kusitishwa

Worldcoin ilisitishwa mnamo Agosti mwaka jana, kufuatia pingamizi la faragha kuhusu kuchanganua mboni za watumiaji ili kubadilishana na kitambulisho cha kidijitali ili kuunda "utambulisho na mtandao mpya wa kifedha"

Muhtasari

• "Tunashukuru kwa uchunguzi wa haki wa DCI na kwa uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kumaliza suala hilo," Scott alinukuliwa katika ripoti hiyo ya Reuters.

Worldcoin
Worldcoin
Image: THE STAR

Shirika linaojihusisha na biashara za pesa za kidijitali, Worldcoin liko huru kurejelea shughuli zao nchini Kenya, karibia mwaka mmoja baada ya shughuli zao kusitishwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Reuters, asasi za usalam nchini Kenya ambazo zilikuwa zinachunguza shughuli zao nchini Kenya.

Mamlaka zilisimamisha Worldcoin mnamo Agosti mwaka jana, kufuatia pingamizi la faragha kuhusu kuchanganua mboni za watumiaji ili kubadilishana na kitambulisho cha kidijitali ili kuunda "utambulisho na mtandao mpya wa kifedha".

Worldcoin inazinduliwa na Tools for Humanity, kampuni iliyoanzishwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa OpenAI Sam Altman. Tovuti yake inasema imesajili watumiaji milioni 5.7 katika zaidi ya nchi 160.

"Baada ya kukagua faili hiyo, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ... aliagiza kwamba faili hiyo ifungwe bila hatua zozote za polisi," Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kenya (DCI) iliandika katika barua ya Juni 14 kwa Coulson Harney, kampuni ya mawakili inayowakilisha Worldcoin kwa mujibu wa ripoti ya Reuters.

Worldcoin itaanza tena usajili wa watumiaji kote nchini Kenya hivi karibuni, alisema Thomas Scott, afisa mkuu wa sheria katika Tools for Humanity, katika taarifa.

"Tunashukuru kwa uchunguzi wa haki wa DCI na kwa uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kumaliza suala hilo," Scott alinukuliwa katika ripoti hiyo ya Reuters.