Inauma sana! Bobi Wine alaani utekaji nyara nchini Kenya

Alilinganisha mtindo wa kutekwa nyara na ule wa Uganda akisema inauma sana kuutazama.

Muhtasari
  • Keter aliripotiwa kutekwa nyara na watu wengine wasiojulikana Jumapili alipokuwa akitoka kwenye hafla ya kanisa eneo la Kileleshwa, Nairobi.
Bobi Wine
Bobi Wine
Image: Facebook

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mwanaharakati, Bobi Wine, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kufuatia visa vya utekaji nyara nchini Kenya hivi majuzi.

Alilinganisha mtindo wa kutekwa nyara na ule wa Uganda akisema inauma sana kuutazama.

"Inauma sana kutazama utekaji nyara wa mtindo wa Uganda ukitokea kwenye mitaa ya Kenya," Bobi Wine alisema katika ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa X.

"Mamlaka huko lazima kupata ushauri mbaya kutoka kwa jirani mbaya," aliongeza.

Kiongozi huyo wa upinzani Uganda alisema kwamba Kenya lazima itetee Katiba yao kabla haijawa dhaifu sana kuweza kuitetea.

"Kama nilivyowaambia kaka na dada zetu nchini Kenya hapo awali, lazima utetee Katiba yako kabla haijawa dhaifu sana kukutetea," Bobi Wine alisema.

Bobi Wine alishiriki video ya aliyekuwa Mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter akitekwa nyara akisema hizo si dalili nzuri.

Keter aliripotiwa kutekwa nyara na watu wengine wasiojulikana Jumapili alipokuwa akitoka kwenye hafla ya kanisa eneo la Kileleshwa, Nairobi.

Kutekwa nyara kwake kunajiri wakati shinikizo zikiongezeka kwa mamlaka kukomesha kuwateka nyara Wakenya wanaopinga utawala wa Kenya Kwanza.

Wiki jana, Chama cha Wanasheria nchini (LSK) na uongozi wa Azimio la Umoja One Kenya walikabidhi ripoti ya watu 39 waliotoweka kutoka kwa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 kwa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai (DCI).

Ruto alipokuwa akijibu ripoti za kukamatwa kwa Keter alisema polisi wana haki ya kwenda na kumkamata yeyote ambaye baada ya kuitwa atakosa kuheshimu.

Hata hivyo, hakuthibitisha kama wito wa kukamatwa ulitolewa kuhusiana na tukio hilo.

"Polisi wakikuita, na ukakataa kwenda, hawana haki ya kuja kukutafuta?" alisema.

"Ikiwa watakuja, je, ni kiasi gani cha kutekwa nyara?" Ruto alikuwa akizungumza katika kikao cha wanahabari katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumapili.

Badala yake aliwapeleka waandishi wa habari polisi ambao alisema ni bora waangaze.

"Badala ya sisi kuwa na msimamo, polisi wametoa taarifa, unaweza kuangalia wametoa nini," alisema.