Rais Ruto aeleza nia ya kujadiliana na vijana kwenye X space

Rais alisema yuko tayari kujadilina na vijana kuhusu masuala yoyote ambayo wanaweza kuwa nayo.

Muhtasari

•Hii inafuatia wito wa wakenya, haswa Gen Z, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ambao wamesema kwamba ikiwa mazungumzo yoyote yatafanyika, yafanywe kwenye X space.

• Katika mahojiano na wanahabari Jumapili, Rais alisema yuko tayari kujadili masuala yoyote ambayo wanaweza kuwa nayo.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: TWITTER

Rais William Ruto ameelezea nia ya kuwashirikisha vijana kwenye mtandao wa X kwenye mazungumzo kuhusu masuala yanayowakumba.

Hii inafuatia wito wa wakenya, hasa Gen Z, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ambao wamesema kwamba ikiwa mazungumzo yoyote yatafanyika na serikali, yafanywe kwenye 

Katika mahojiano na wanahabari siku ya Jumapili, Rais alisema yuko tayari kujadili masuala yoyote ambayo wanaweza kuwa nayo.

“Nasikia vijana wanasema hawataki jukwaa  la wadau wengi ,labda tufanye mazungumzo na rais kwenye X. Mimi niko wazi kufanya mazungumzo na vijana kwenye jukwaa wanalostarehe nalo. Wakitaka nishirikiane nao kwenye X, nitakuwepo," Rais Ruto alisema.

Aliongeza, "Nataka tujadili kuhusu kodi, nataka tujadili ukosefu wa ajira, rushwa na masuala yote."

Vijana wamekuwa wakiandaa maandamano nchini kote kwa muda wa wiki mbili kuhusu mswada wa fedha wa 2024, ambao Ruto aliondoa kufuatia shinikizo iliyoongezeka.

Hata hivyo,rais  alithibitisha ufahamu wake kuhusu changamoto za vijana na kuahidi kushughulikia matatizo yao kwa kina.

"Nina vijana nyumbani, na ninajua wasiwasi wao," alisema.

Jukwaa la X Space hivi majuzi limekuwa na shughuli kali, huku vijana wakilitumia kutoa maoni yao kwenye X Space, ambayo wanataka rais ashughulikie.