Polisi wamuokoa mshukiwa wa wizi kutokana na kuuawa na waandamanaji Mombasa

Katika video, mwanamume huyo aliyevalia shati jeusi anaonekana akipigwa na waandamanaji kabla ya kutoroka.

Muhtasari
  • Hii ilikuwa baada ya kudaiwa kunaswa na waandamanaji wanaoipinga serikali mjini Mombasa akijaribu kuiba.

Polisi mjini Mombasa mnamo Jumanne waliingilia kati kumwokoa mshukiwa wa mwizi kutokana na kuuawa.

Hii ilikuwa baada ya kudaiwa kunaswa na waandamanaji wanaoipinga serikali mjini Mombasa akijaribu kuiba.

Katika video, mwanamume huyo aliyevalia shati jeusi anaonekana akipigwa na waandamanaji kabla ya kutoroka.

Hata hivyo anakamatwa tena na kupigwa kabla ya polisi kuingilia kati na kumuokoa.

Kisha mshukiwa anaokolewa na maafisa wa polisi waliomchukua kwa land cruiser na kuondoka naye.

Maandamano yalianza mapema mjini Mombasa huku waandamanaji wa amani wakiimba nyimbo za kuipinga serikali na kubeba mabango.

Wakati fulani, vikundi vya waandamanaji wa amani mjini Mombasa vilijigawanya katika makundi mawili huku wahuni wakijinufaisha na kuanza kuwahangaisha waandamanaji.