Tutawasaidia waliojeruhiwa na kuuawa wakati wa maandamano- Ruto

Akihutubia taifa siku ya Ijumaa, Ruto alitoa rambirambi zake kwa wote waliopoteza maisha.

Muhtasari
  • Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya kuandaa mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri kuhusu maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha.
Image: screengrab

Rais Wiliam Ruto amesema serikali itawaunga mkono waliopoteza maisha na kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha 2024.

Akihutubia taifa siku ya Ijumaa, Ruto alitoa rambirambi zake kwa wote waliopoteza maisha.

"Kwa wengine wengi waliopoteza maisha, natuma risala za rambirambi kwa familia," alisema.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya kuandaa mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri kuhusu maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha.